Uko Offline kwa sasa. Unaweza kuendelea kuona mfumo, lakini Login, Usajili, na kuhifadhi taarifa vinahitaji mtandao.
Karibu Ndani ya SmartDuka Security!
Mtumiaji mpya aliyejisajili atapata Ofa ya Wiki 1 Bure kwa ajili ya
kutumia na kuona kama mfumo huu unamfaa katika biashara yake.
Baada ya wiki moja kuisha, utahitajika kulipia kifurushi cha muda wako unaotaka ili
kuendelea kutumia mfumo bila kusumbuliwa. Tunatumaini utafurahia huduma zetu!
Ongeza bidhaa zako na stock ya kuanzia.
Fanya mauzo (POS) na mfumo utahesabu faida yenyewe.
Tunza wadaiwa na uwakumbushe moja kwa moja WhatsApp.
Pata ripoti kamili ya biashara yako wakati wowote.
Taarifa Zako Za Awali Zipo!
Tuligundua kuwa uliwahi kuingiza taarifa za biashara yako (bidhaa, mauzo, madeni au matumizi)
kabla ya kutoka (logout). Unataka kuendelea na taarifa hizo au kuanza upya?
SmartDuka Security
Manage Smart, Grow Secure.
Mfumo mmoja unaokupa udhibiti kamili wa stock, mauzo, wadaiwa, matumizi, ripoti, na ulinzi wa biashara yako - popote ulipo, wakati wowote, hata bila mtandao.
Kila Kitu Unachohitaji Kudhibiti Duka Lako - Mahali Pamoja
SmartDuka Security si "kitabu cha kuandikia" cha kawaida - ni mfumo kamili unaofanya kazi ngumu badala yako, hivyo unabaki na muda zaidi wa kukuza biashara yako.
Udhibiti Kamili wa Stock
Ongeza bidhaa na bei zake (rejareja na jumla), mfumo unakuonyesha stock iliyobaki papo hapo na kukutahadharisha bidhaa inapokaribia kuisha - huhitaji tena kuhesabu kwa mkono.
Mauzo (POS) Rejareja na Jumla
Fanya mauzo kwa mbofyo michache - mfumo unapunguza stock na kuhesabu faida yenyewe kila mara unapouza, bila makosa ya hesabu za mkono.
Wadaiwa na Ukumbusho wa WhatsApp
Tunza orodha kamili ya wanaokudai, kiasi, na namba zao - kisha uwatumie ukumbusho wa malipo kupitia WhatsApp kwa mbofyo mmoja.
Ufuatiliaji wa Matumizi
Rekodi gharama na matumizi ya kila siku ya duka lako, ili ujue kwa uhakika faida yako halisi baada ya gharama zote.
Ripoti za Papo Kwa Papo + PDF
Ona jumla ya mauzo, madeni, matumizi, na faida ya biashara yako wakati wowote, kisha pakua ripoti kamili kama faili la PDF la kitaalamu.
Uchambuzi wa Kitaalamu wa Kila Mwezi
Mfumo unakuonyesha bidhaa inayouzika zaidi na ile "imelala" bila kuuzwa (dead stock), kisha unakupa ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kuongeza mauzo yako.
Ulinzi wa Hali ya Juu (Security)
Kila shughuli inarekodiwa (Audit Trail), akaunti zinalindwa kwa nenosiri salama, na Admin ana uwezo wa kufuatilia matukio yote ya mfumo wako wakati wowote.
Fanya Kazi Popote - Hata Bila Mtandao
Sakinisha (Install) mfumo kwenye simu au kompyuta yako kama app halisi, badilisha lugha kati ya Kiswahili na English, na uendelee kuutumia hata ukiwa na mtandao dhaifu.
Jinsi Inavyofanya Kazi - Hatua 3 Tu
1
Jisajili Bure
Chukua sekunde chache tu kujisajili - unapata Wiki 1 Bure ya kujaribu mfumo kikamilifu bila malipo.
2
Ongeza Bidhaa Zako
Weka bidhaa, bei, na stock ya kuanzia ya duka lako - mfumo uko tayari kuanza kufanya kazi papo hapo.
3
Anza Kuuza na Kufuatilia
Fanya mauzo, fuatilia wadaiwa na matumizi, kisha uangalie ripoti na ushauri wa kitaalamu ukikua kila mwezi.
Data yako inalindwa kwa teknolojia salama ya Firebase
Huduma ya Wiki 1 Bure kwa kila mtumiaji mpya
Msaada wa moja kwa moja wa Admin kupitia WhatsApp
Soma Vidokezo vya Biashara kwenye Blog Yetu
Makala za mara kwa mara kuhusu jinsi ya kukuza duka lako, kudhibiti stock vizuri, na kutumia SmartDuka Security kwa ufanisi zaidi.
Uko Tayari Kuanza Kudhibiti Duka Lako Kisasa Zaidi?
Weka email yako ya usajili. Tutakutumia link ya kubadili nenosiri moja kwa moja kwenye email yako.
Angalia Email Yako Sasa!
Tumekutumia link ya kubadili password. Fungua Gmail yako na iangalie
juu kabisa ya orodha ya email (Inbox) - hapo ndipo utakapoiona link hiyo mara nyingi.
Kama huioni juu kwenye Inbox: bonyeza vishale vitatu (☰)
vilivyopo upande wa kushoto juu kwenye Gmail yako, kisha tafuta na ubonyeze sehemu iliyoandikwa
"Spam". Ndani ya Spam ndipo utakapoikuta email hiyo yenye namna ya kujaza
taarifa zako za kubadili password yako upya.
Ukiikuta kwenye Spam, ifungue kisha fuata maelekezo yaliyomo ndani kukamilisha
kubadili password yako kwa usalama.
Maombi ya Addition Service (Uchambuzi wa Mwezi - Tsh 1,000)
Hakuna maombi kwa sasa...
Usimamizi wa Makala (Articles / Blog)
Makala Zilizopo
Kichwa
Hali
Tarehe
Action
Global System Broadcasting
Password Reset Log (Maombi ya Password)
Advanced Audit Trail Filter
Hakuna tukio lililorekodiwa bado...
Jina la Duka
Karibu kwenye mfumo wako wa usimamizi wa duka na ulinzi wa biashara.
Wasiliana na Msimamizi wa Mfumo
Una tatizo, swali, au unahitaji msaada wowote kuhusu mfumo wako? Piga namba iliyopo hapa chini.
0752 405 422
Onboarding / Hatua za Kufuata
Nenda kwenye tab ya Bidhaa uongeze bidhaa na stock ya kuanzia.
Nenda kwenye tab ya New Sales (POS) kufanya mauzo kwa urahisi.
Mfumo utapunguza stock na kuongeza pesa kwenye ripoti kiotomatiki.
Angalia Reports & Sync kutuma au kupakua ripoti yako.
Angalia Maendeleo mwisho wa mwezi kupata ushauri wa kitaalamu wa biashara yako.
Ongeza Bidhaa Mpya
Tahadhari ya Stock (Inaisha)
Orodha ya Bidhaa Zote:
Fanya Mauzo Hapa (POS)
Kikapu cha Mauzo / Hali ya Sasa
Uza bidhaa kwa usahihi wa hali ya juu na mfumo utafanya hesabu yenyewe.
Historia ya Mauzo Yote
Sajili Mdaiwa wa Moja kwa Moja
Wadaiwa Waliopo:
Rekodi Gharama/Matumizi
Orodha ya Matumizi:
Ripoti ya Biashara
Jumla ya Mauzo:Tsh 0
Jumla ya Mtaji wa Bidhaa zilizopo:Tsh 0
Jumla ya Madeni:Tsh 0
Jumla ya Matumizi:Tsh 0
Makadirio ya Faida:Tsh 0
Backup & Ripoti Yako
Pakua ripoti kamili ya duka lako kama faili (PDF) kwenye kifaa chako wakati wowote.
Uchambuzi wa Kila Mwezi wa Biashara Yako
Kila mwisho wa mwezi, mfumo unakuchambulia ni bidhaa gani inauzika sana na ipi imekaa
muda mrefu bila kuuzwa (dead stock), kisha unakupa ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya
kuboresha mauzo yako.
Hii ni Huduma ya Ziada (Addition Service) ya
Tsh 1,000 / mwezi. Bado haijawashwa kwenye akaunti yako.
Blog ya SmartDuka Security
Vidokezo, ushauri, na habari za hivi karibuni kuhusu kukuza na kulinda biashara yako.
Hakuna makala yaliyochapishwa kwa sasa. Rudi baadaye.
Masharti na Vigezo vya Matumizi
Tafadhali soma na kukubali ili kuendelea kutumia SmartDuka Security.
Karibu kwenye SmartDuka Security. Kabla ya kuanza kutumia huduma zetu za kusimamia duka lako, stoo, na ripoti za biashara yako, lazima ukubali masharti haya ya matumizi:
1. Umiliki wa Data na Usalama
Data zote unazoingiza (mauzo, bidhaa, na taarifa za wateja) ni mali yako. SmartDuka Security inahakikisha ulinzi na usalama wa data hizo na hazitashirikishwa kwa namna yoyote ile bila idhini yako kimaandishi.
2. Matumizi Halali ya Mfumo
Unakubali kutumia mfumo huu kwa ajili ya biashara halali pekee. Ni marufuku kuingiza taarifa za uongo, kufanya miamala ya kitapeli, au kujaribu kushambulia kiusalama miundombinu ya mfumo huu.
3. Huduma ya Premium na Malipo
Ufikiaji wa ripoti maalumu za faida, hasara, na dashboards za kiutawala unaweza kuzuiliwa kulingana na kifurushi cha usajili wako (Premium Subscription). Mtumiaji anapaswa kulipia huduma kwa wakati ili kuepuka kusitishiwa ufikiaji wa ripoti hizi muhimu.
4. Ulinzi wa Akaunti Yako
Mtumiaji anawajibika kulinda neno lake la siri (password). SmartDuka Security haitahusika na upotevu wa data uliosababishwa na uzembe wa mtumiaji kutoa password yake kwa watu wasiohusika.
5. Marekebisho ya Huduma
Tuna haki ya kuboresha, kubadilisha au kusitisha sehemu fulani ya huduma ili kuongeza ufanisi wa mfumo. Mabadiliko makubwa yatatolewa taarifa kupitia ndani ya mfumo.
Privacy & Policy
Faragha na Usalama wa Taarifa Zako - SmartDuka Security.
Karibu SmartDuka Security. Sisi tunathamini na kulinda faragha ya taarifa za biashara yako na wateja wako. Sera hii inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia na kulinda data zako.
1. Taarifa Tunazokusanya
Tunakusanya taarifa unazoingiza mwenyewe kama: jina la duka/mmiliki, email, namba ya WhatsApp, bidhaa, mauzo, wadaiwa na matumizi ya biashara yako, kwa lengo la kukuletea huduma bora za usimamizi wa duka.
2. Matumizi ya Taarifa Zako
Taarifa zako zinatumika tu kuendesha akaunti yako, kukuletea ripoti sahihi za biashara, kukukumbusha kuhusu vifurushi vyako, na kuboresha huduma zetu. Hatuuzi wala kushirikisha data zako na mtu au kampuni ya tatu bila idhini yako.
3. Usalama wa Data
Mfumo unatumia teknolojia salama (Firebase Security) kuhifadhi taarifa zako. Hata hivyo, ni wajibu wako pia kulinda password yako na kutokuishirikisha na watu wasiohusika.
4. Mawasiliano na Admin
Kwa maswali, malalamiko au msaada wowote kuhusu faragha ya taarifa zako, unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Msimamizi wa Mfumo kupitia namba: 0752 405 422.
5. Mabadiliko ya Sera
Tunaweza kubadilisha sera hii ya faragha wakati wowote ili kuendana na maboresho ya mfumo. Mabadiliko makubwa yatatolewa taarifa ndani ya mfumo.
Rules & Regulations
Kanuni na Muongozo wa Matumizi Bora ya SmartDuka Security.
Kanuni hizi zimewekwa kulinda mmiliki wa mfumo wa SmartDuka Security na kukuongoza wewe mtumiaji kutumia mfumo huu kwa usahihi na kwa mujibu wa sheria.
1. Matumizi Halali Pekee
Ni marufuku kutumia mfumo huu kuendesha biashara haramu, kuficha mapato kwa nia ya udanganyifu, kuiba taarifa za wengine, au kufanya shughuli yoyote inayokiuka sheria za nchi.
2. Usahihi wa Taarifa
Mtumiaji anawajibika kuingiza taarifa sahihi za bidhaa, mauzo na wadaiwa. Mmiliki wa mfumo hatawajibika na hasara itokanayo na taarifa za uongo ulizoziweka mwenyewe.
3. Marufuku ya Kushambulia Mfumo
Ni marufuku kujaribu kuvunja, kudukua (hack), kunakili msimbo wa mfumo, au kuutumia mfumo huu kwa njia inayolenga kuudhuru au kuudhoofisha kiusalama.
4. Wajibu wa Malipo
Baada ya kipindi cha Trial cha wiki moja kuisha, mtumiaji anatakiwa kulipia kifurushi husika ili kuendelea kutumia mfumo. Kutolipa kutasababisha ufikiaji wa mfumo kuzuiliwa moja kwa moja.
5. Haki ya Mmiliki wa Mfumo
Mmiliki wa SmartDuka Security ana haki ya kuzimisha akaunti yoyote inayokiuka kanuni hizi, kuboresha mfumo, au kusitisha huduma kwa taarifa ndani ya mfumo, bila kuathiri haki za msingi za mtumiaji mwadilifu.
6. Msaada na Mawasiliano
Kwa ufafanuzi zaidi wa kanuni hizi au kuripoti tatizo lolote, wasiliana na Msimamizi wa Mfumo kupitia namba: 0752 405 422.